Écoutez le conte : Siku ile jangwa la sahara litasitawi tena
Publié le :
Écouter - 03:53
Sikiliza upepo, hii ni Sahara inayolia. Inataka kusitawi tena.
Sikiliza upepo, hii ni Sahara inayolia. Inataka kusitawi tena.
Sahara haikuwa daima nyika. Ilikuwa inchi nzuri ya kijani. Wakaazi wake wameheshimu maumbile. Wameishi huko na wamefurahia. Wamezalisha wanyama, wamelima na wamewinda. Wameipenda ardhi yao na ardhi yao imewapenda. Basi walitokea watu wenye tamaa na maafa yakaenea popote.
Watu hawa hawakutaka mali ila ardhi. Na kiasi chochote cha ardhi hakikuwaridhisha, daima walitamani zaidi. Na walipowinda, wameuwa, siyo kwa ajili ya kitoweo chao lakini kwa kuonyesha ujasiri wao. Wameharibu misitu, siyo kwa kujihifadhi na mvua au jua lakini kwa kujenga majumba makubwa. Watu hawa wasio na maadili wakaijerui sana Sahara hata ikawa nyika. Bado watu wake wanaonyesha upendo walio nao kwake na kukaa bila kuhama. Sahara imeguswa. Kwa kuwashukuru kwa ajili ya upendo wao, imewapa oasisi na kingo za mto mkubwa Niger.
Lakini hata hivyo, inaendelea kuwa bila furaha.
Sikiliza upepo, hii ni Sahara inayolia. Inataka kusitawi tena.
Siku moja akatokea mtu mwenyi busara. Sahara ikamuuliza: Nitapataje uelewano niliyoufaamu kabla? “Kumbatia watu waaminifu na wenyi fahari, watu waheshimuo umbile. Siku moja, atatokea mtu mmoja. Atapulizia uhai juu ya majani na miti uliyoifaamu. Mtu huyu ana mbegu zitakazokufanya uchanue tena.” Huyu ni mtu mwadilifu. Atatoa uhai wake kwa ajili ya mimea yenu”. Lakini kudai pepo yako iliyopotea, lazima awatupilie mbali watu wenye tamaa. Na hii itakuwa kweli kazi ngumu. Bahati nzuri, mtumishi mwaminifu atamsaidia kushinda vikwazo na maadui wake. Mtu huyu anazo mbegu zitakazokufanya usitawi tena.
Sikiliza upepo, hii ni Sahara inayolia. Inataka kusitawi tena.
Inasubiriwa mtu mwadilifu kuifanya iwe ya kijani tena.
Zaidi utaheshimu Mama Umbile, ndivyo utakavyompenda, na kulifanya njangwa kusitawi haraka iwezekanavyo.